Mnamo tarehe 22.11.2024
Jeshi la Polisi la mkoani Songwe liliripoti kuwakamata Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, mwanasiasa wa CHADEMA, Joseph Mbilinyi (Sugu), pamoja na viongozi wengine waliokuwa katika msafara wa CHADEMA.
Jeshi la polisi likidhibitisha kukamatwa kwao, Askofu Emmaus B Mwamakula, amekashifu kitendo hicho na kusema kuwa ni ukiukaji wa uhuru wa kuendesha kampeni, huku akitoa wito kuachiwa kwa viongozi hao.
Na baada ya masaa kadhaa kupita, majira ya usiku jeshi la polisi la mkoani songwe liliwaachia huru viongozi hao bila masharti yeyote.
Kwamujibu wa mkurugenzi wa Itifaki, mawasiliano na mambo ya nje wa CHADEMA Jon Mrema amesema “Mdude hajaachiwa, RPC Kasema Wana mahojiano naye pamoja na Mtu mmoja ambaye aliumizwa vibaya na Polisi, tunaendelea kufuatilia hali ya afya ya Mdude”
Aidha viongozi waliokamatwa ni Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe, Joseph Mbilinyi (Sugu) Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Pascal Yohana Haonga, Mbunge Mstaafu CHADEMA Mbozi Mlowo, Mdude Mpaluka Nyagali, Apolinary Boniface Margwe, Afisa Habari CHADEMA na Adam Hassan Kasekwa, Mlinzi wa Mwenyekiti wa CHADEMA. Wengine waliokamatwa ni Paul Joseph Paul, Afisa wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mbeya, Kelvin Keneth Ndabila, Afisa habari Kanda ya Nyasa, Mkazi wa Mbeya, Michael Laison Msongole, Mwenyekiti CHADEMA Wilaya ya Mbozi, Mlowo, Mohamed Abdilah Ling wanya, Mlinzi wa Mbowe Mkazi wa Dar es salaam, Alfan Hassan Mbire, Mlinzi wa Mbowe na Ezekia Elia Zambi, Mwenyekiti ACT Wazalendo Mkoa wa Songwe.
Siku ya jana Novemba 22,2024 viongozi hao wa CHADEMA walikamatwa na polisi stendi ya zamani ya Mlowo Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe majira ya 10:30 asubuhi baada ya kwenda kufanya mkutano wa kampeni eneo ambao hawakupangiwa na ndipo Askari waliwapa amri ya kutawanyika lakini walikaidi na askari waliamua kuwatawanya kwa nguvu na ndipo walipoanza kurusha mawe na kuwajeruhi Askari wawili maeneo ya kichwani, usoni na puani na kwa sasa wanaendela na matibabu Hospitali ya Wilaya ya Mbozi”
d”
