
Mara nyingi katika mada zangu nimekuwa nikizungumzia namna ya kutibu maradhi mbalimbali yanayomkwamisha mwanadamu kushiriki ipasavyo kazi za ujenzi wa taifa.
Tiba ninazozungumzia ni zile asili zisizoacha athari mbaya kwenye mwili wa mgonjwa. Leo nimeona nizungumzie namna ya kujikinga dhidi ya majipu.
Kinga hiyo ni mbegu za nyonyo au mbono.
Chukua mbegu hizo, ni vema ziwe zile ndogo zenye ukubwa wa kidonge, meza moja asubuhi, moja mchana na nyingine jioni muda wa siku tano. Rudia dozi hii baada ya miezi minne. Hii ni kinga nzuri hususan kwa anayeotwa majipu mara kwa mara.
Majipu pamoja na kumsababishia mgonjwa maumivu makali pia yanamwacha na makovu ambayo huchukua miaka mingi kuondoka katika ngozi yake.
Kimsingi jipu au majipu husababishwa na vijidudu wanaojulikana kama ‘stafilokokasi’ ambao huingia kwenye vijifuko vya jasho kupitia vinyweleo vya mwili. Jipu ni uvimbe unaoanza sehemu maalumu.
Linaweza kuwa jipu moja au zaidi. Uvimbe wa jipu hukua na kisha kutunga usaa ambao hutumbuka. Mwanzo jipu huwasha na kisha huwa na maumivu makali hasa linapoota sehemu ambayo ngozi yake imebana kama puani , sikioni, kwapani au katikati ya kidole.
Mara nyingi chanzo cha jipu ni sumu ndani ya mfumo wa damu inayosababishwa na kutokula vyakula vinavyostahili mwilini.
Kama una tatizo lolote la kiafya, karibu kwenye kituo chetu cha kutolea huduma za afya, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam. Acha kuendelea kuteseka kwa maradhi yaliyoshindikana.
Tunamjali mgonjwa yeyote, tunatumia tiba lishe na virutubisho asili kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiafya zinazomsumbua binadamu.
Pia unaweza kunipigia kwa 0745900600 iwapo unataka ufafanuzi wa jambo au namna ya kufika katika kituo chetu. Au niandikie kupitia barua pepe dkmandaitz@gmail.com. Au tembelea televisheni yetu MANDAI TV ONLINE, utajifunza mambo mengi yanayohusu afya yako.
