
Mtaalam wa virutubisho tiba, Abdallah Mandai amesema mama anayesumbuka kutafuta mtoto atumie mchanganyiko wa tende na maziwa ya mbuzi ni tiba mujarabu ya tatizo hilo.
“Chukua tende ujazo wa kiganja cha mkono, loweka katika maziwa ya mbuzi kwa siku nzima, pekecha tende ndani ya maziwa hayo, chukua unga wa iriki na asali, changanya pamoja.
“Kunywa mchanganyiko huo saa moja kabla ya kwenda kulala. Mchanganyiko huu ni mujarabu sana, unasisimua na kuimarisha mbegu za uzazi,” amesema mtaalam Mandai leo Jumanne Septemba 27, 2022, jijini Dar es Salaam.
Aidha, ametoa mwito kwa wenye matatizo ya aina yoyote ya kiafya kwenda kwenye kituo chake cha kutolea huduma za afya Ukonga Mongolandege, jijini Dar es Salaam au wampigie simu kwa namba 0745900600 iwapo wanataka ufafanuzi wa jambo au namna ya kufika katika kituo hicho.
