
Marekani imetangaza kuwa inapeleka chanjo milioni 2.5 za COVID-19 nchini Taiwan, ikiongeza kwa kiasi kikubwa ahadi yake ya awali ya kutuma dozi 750,000.
Tangazo hilo linakuja wakati takribani asilimia 45 ya wamarekani wamepatiwa chanjo kamili dhidi ya virusi vya Corona kulingana na kitengo kinachofuatilia virusi vya Corona kutoka chuo kikuu cha John Hopkins cha Marekani
Rais wa Taiwan, Tsai Ing-wen amesema kuongezeka kwa idadi ya dozi, ni ishara ya urafiki unaosonga mbele.
Rais wa Marekani Joe Biden amesema utawala wake utasambaza chanjo milioni 80 kote duniani.
Dozi hizo ni sehemu ya msaada wa dozi milioni 500 ambazo Marekani imejitolea kuchangia kwa takribani maeneo 100 kwa zaidi ya miaka miwili ijayo.
Utawala wa Biden unapanga kuchangia dozi milioni 200 mwaka huu na nyingine milioni 300 katika mwaka 2022 kwenda nchi 92 pamoja na Umoja wa Afrika.
Tangazo linakuja wakati takribani asilimia 45 ya wamarekani wamepatiwa chanjo kamili dhidi ya virusi vya Corona kulingana na kitengo kinachofuatilia virusi vya Corona kutoka chuo kikuu cha John Hopkins cha Marekani.
Wakati huo huo, Marekani pekee ina zaidi ya kesi milioni 33.5. Virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.
