Habari mbaya za kusikitisha zilizotufikia jana zinaeleza kuwa mama wa msanii Hawa Hussen almaarufu Carina, Fatma Maruzuku amefariki dunia.
Mama Carina amefariki yapata siku arobaini tangu alipofariki mwanaye Carina.
Habari za kifo cha mama wa Carina zimethibitisha na mmoja wa wanafamilia aliyeongea na Mandai TV dakika chache zilizopita.
Mama Carina alikuwa anasumbuliwa na presha na kisukari na hakuweza hata kushiriki arobaini ya mwanaye wiki iliyopita.
Picha: Global Publishers
