
Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Rwanda, Paul Kagame katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kigali nchini Rwanda. Yupo nchini humo katika Jukwaa la Wakulima kwenye Mkutano wa Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika wa mwaka 2022 (AGRF 2022) uliofanyika Kigali nchini Rwanda jana Septemba 6, 2022.

