
Uongozi wa mkoa wa Tabora umeushukuru Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), pamoja na wanachama wake kwa kuchagua shughuli za Maadhimisho ya Juma la Elimu kitaifa mwaka huu 2022, kufanyika wilayani Igunga.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora kupitia, kwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Sauda Mtondoo, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Dk. Batilda Buriani.
Akizungumza katika hotuba ya uzinduzi huo amessema wanaushukuru Mtandao wa Elimu, TENMET kwa kuichagua Igunga kuwa sehemu ya kufanyia shughuli hizo za kielimu.
Aliongeza kuwa shughuli za maadhimisho hayo zinatoa fursa muhimu ya kutafakari kwa pamoja jinsi ya kuendelea kuondoa vikwazo vya ujifunzaji na uimarishaji wa elimu kwa kiwango cha ujenzi wa umahiri/ujuzi wa utendaji.
Awali kwa upande wake, Mratibu wa TEN/MET, Ochola Wayoga akizungumzia shughuli za maadhimisho kwa mwaka huu, alisema wamedhamiria kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kuchangia uboreshaji wa elimu nchini.
Pia kuhamasisha na kukumbusha jamii, serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau mbalimbali wa elimu kuhusu umuhimu wa uchangiaji wa elimu kwa kuzingatia kauli mbiu ‘Gharamia Elimu Bora Kuboresha Matokeo ya Ujifunzaji: Elimu Kwanza.
“Pamoja na hayo, ni kuhamasisha serikali kuboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia na pia kuzingatia makundi yaliyokosa fursa kama watoto wenye ulemavu, watoto wakike na makundi mengine maalumu,” Wayoga.
Hata hivyo, aliishukuru serikali kuu kupitia ofisi ya Raisi TAMISEMI na mkoa kwa kutoa kibali cha kufanyika kwa maadhimisho hayo ya Juma la Elimu kitaifa mkoani Tabora hasa katika wilaya ya Igunga.
