
Mtaalam wa virutubisho tiba, Abdallah Mandai amesema kitunguu swaumu ni tiba anuai ya maradhi ya kichomi.
“Ponda punje 10 za kitunguu swaumu hadi ziwe kama ujiuji, ongeza robo glasi ya maji na asali kijiko kimoja cha mezani.
“Changanya vizuri mpe mgonjwa wa kichomi anywe na mpake kitunguu swaumu sehemu za kifua zenye maumivu.
“Endelea kumpa mgonjwa tiba hii kila siku asubuhi na jioni muda wa siku saba,” amebainisha hayo mtaalam Mandai, leo Jumatano Agosti 24, 2022 jijini Dar es Salaam.
Aidha, kwa mwenye tatizo lolote la kiafya Mandai anamkaribisha kwenda kupata huduma kwenye kituo chake cha kutolea huduma za afya, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane naye simu namba 0745900600.
