
Mtaalam wa virutubisho tiba, Abdallah Mandai, amesema juisi ya kitunguu husaidia jipu kuiva haraka kwa mwenye tatizo.
“Changanya juisi ya kitunguu maji na swaumu yenye kiasi kinacholingana inayotosha kupaka kwenye jipu siku nzima, ipake katika jipu mara kwa mara kutwa nzima.
“Mchanganyiko huu pamoja na mambo mengine unasaidia kuivisha haraka jipu na kuponyesha jeraha baada ya kutumbuka,” amebainisha hilo mtaalam Mandai leo Jumatano, Agosti 31, 2022, jijini Dar es Salaam.
Amesema baada ya jipu kutumbuka mgonjwa aendelee kuosha kidonda na kupaka mchangayiko huo, unasaidia kukiponyesha kwa haraka zaidi.

Amefafanua kuwa mara nyingi chanzo cha jipu ni sumu ndani ya mfumo wa damu inayosababishwa na kutokula vyakula vinavyostahili kwa mwili.
Aidha, ametoa mwito kwa yeyote mwenye tatizo la kiafya kwenda katika kituo chake cha kutolea huduma Ukonga Mongolandege, jijini Dar es Salaam au ampigie simu namba 0745900600.
