Mgombea mwenza wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema kuwa serikali ijayo inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuimarisha diplomasia ya uchumi, hususan kwa mataifa jirani na Tanzania, ili kufungua zaidi fursa za biashara mipakani.
Dkt. Nchimbi alitoa kauli hiyo, Oktoba 12, wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika wilayani Kakonko, mkoani Kigoma.
Akiwa katika muendelezo wa kampeni za urais kupitia CCM, alisisitiza dhamira ya serikali ijayo kuendeleza ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi na nchi jirani, ili kuongeza pato la taifa na kuboresha maisha ya wananchi.
