Mgombea Mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema kuwa chama hicho kimekuwa na desturi ya kutekeleza ahadi zake kwa wakati, na hivyo wananchi wa Wilaya ya Kwimba, Mkoa wa Mwanza, wanapaswa kutarajia huduma ya maji safi na salama.
Dkt. Nchimbi alibainisha kuwa CCM imedhamiria kuongeza kasi ya upatikanaji wa maji, hatua itakayowarahisishia wananchi maisha ya kila siku na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Amesema chama hicho kimeendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya kijamii kwa vitendo na si kwa maneno pekee, jambo linaloendelea kujenga imani kwa Watanzania.
