Mgombea mwenza wa kiti cha Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ameahidi upanuzi wa maegesho katika Kivuko cha Magogoni na Kigamboni ili kupunguza foleni na kuboresha huduma kwa wananchi.
Akizungumza na wananchi wa Kigamboni katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, Dkt. Nchimbi amesema pia serikali itaharakisha matengenezo ya vivuko vya MV Magogoni na MV Kigamboni katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Dkt. Emmanuel John Nchimbi ni mgombea mwenza wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakipeperusha bendera ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2025, huku mkoa wa Dar es Salaam ukiwa wa 15 kufikiwa na Dkt. Nchimbi katika kusaka kura za ushindi kwa chama hicho tawala.
