Mwenyekiti wa Bodi ya Jukwaa la Katiba (JUKATA) Dkt. Ananilea Nkya amesema siasa zimebadilika nchini na watu wengi wamekuwa wanasiasa wa kusifia kupindukia (siasa za kichawa), siasa za wenye fedha na wenye nafasi.
Dkt. Nkya ameyasema hayo leo Septemba 15, 2025 alipokuwa akichangia mada kwenye maadhimisho ya Siku Kimataifa ya Demokrasia yaliyoandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) akieleza kuwa ni mwanaume au mwanamke asiyejiheshimu pekee ndiye ataamua kuwa chawa.
“ni mwanamke asiyejiheshimu tu ndiye atakuwa chawa wa mtu, na ni mwanaume asiyejiheshimu tu asiyetambua thamani yake ndiye atakubali kuwa chawa” amesema Dkt. Nkya
Aidha ameeleza kuwa mazingira ya kisiasa kwa wanawake hasa kwa vyama vya upinzani ni magumu jambo lilalowafanya wanawake kuwa wagumu kukubali kufanya siasa katika vyama hivyo.
