
Idadi ya maambukizi mapya ya virusi vya ugonjwa wa Covid 19, imeongezeka na kufikia watu 161 ikilinganishwa na 68 waliokuwapo kati Aprili 2 hadi Mei 4, 2022.
Mganga mkuu wa Serikali, Aifello Sichalwe katika taarifa yake iliyotolewa jana Juni 7, 2022, imesema ongezeko hilo ni sawa na asilimia 137.
Hata hivyo, Dk. Sichalwe amesema katika kipindi cha miezi miwili, hakuna kifo kilichotokea kutokana na ugonjwa huo.
Amesema katika kipindi cha Mei 5 hadi Juni 3, 2022 inaonesha mkoa wa Dar es Salaam una wagonjwa 130, Arusha 10, Mwanza 5, Mtwara 4, Dodoma 2, Mara 2, Morogoro 2, Kilimanjaro 1, Simiyu 1, Katavi 1 na Mbeya 1.
Aidha, wagonjwa watatu waliolazwa hawakuwa wamepatiwa chanjo ya Uviko 19 ambayo imeonesha watu kuwa na kinga dhidi ya ugonjwa huo.
Dk. Sichalwe amesema kati ya Mei 5 na Juni 3 watu 775,680 wamapatiwa chanjo ya Uviko 19 nchini, hivyo amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kupata chanjo hiyo.
