
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dakta Hussein Ali Mwinyi, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Shirikisho la Ujerumani Nchini Tanzania, Regine Hess.
Dakta Mwinyi alikutana na Balozi Regine jana Ikulu ya Zanzibar akiwa na ujumbe wake.
Pamoja na mambo mengine mazungumzo baina ya Rais Dakta Mwinyi na Balozi Hess yalilenga kukuza uhusiano baina ya visiwa hivyo na Ujerumani.
