Ofisa wa Jeshi la Polisi aliyekuwa na cheo cha Stesheni Sajenti (Ssgt), Meshack Samson, ambaye alipandishwa kutoka sajenti mwaka 2019, baada ya kukataa rushwa ya sh. milioni 10 ameshushwa.
Askari huyo ameshushwa cheo kutokana na kutotii Mamlaka ya kwenda Kozi ya Kipolisi kuendana na Cheo alichopewa, ikielezwa hakuwa na sababu za msingi kukataa kufanya hivyo.
Ameshushwa ngazi moja kutoka Stesheni Sajenti kuwa Sajenti wa Polisi baada ya kushtakiwa na kupatikana na hatia ya utovu wa nidhamu kwa kukataa amri halali ya Mkuu wa Jeshi la Polisi.


