M – Mama ni huduma ya usafiri wa dharura kwa mama mjamzito aliye na dharura ya uzazi lakini pia kwa mama ambaye ameshajifungua ndani ya siku 42 akipata dharura yoyote ya kiafya. Pia kwa mtoto mchanga aliye ndani ya siku 28. M-Mama ni huduma inayotolewa na Serikali.
Akizungumza na wanahabari Simon Nzilibili ambaye ni Mratibu wa Hamasa ya huduma ya M- Mama Wizara ya Afya alisema kuwa
“Ni lazima mama anapofika kliniki apate elimu ya afya ya uzazi. Ukiachana na suala la M- Mama lakini kuna huduma na elimu nyingi anaipata lakini kwa sasa kuna package hii ya M – Mama nayo imeongezeka kwahiyo anapofika pale pia anapata elimu ya huduma ya M – Mama akipata dharura hata kama akiwa nyumbani afanye kitu gani”.
“Tunashukuru Serikali huduma za mama mjamzito zipo kwenye level ya chini, kuanzia zahanati mpaka kwenye level ya hospitali ya Taifa. Hivyo mama mjamzito anaweza akapata huduma kuanzia kliniki hadi kujifungua”.
“Lakini pia inategemea kwa sababu kuna condition tofauti tofauti kwa mfano kwa mama ambaye amejifungua kwa operesheni kwa mimba ya kwanza hao ndio hawawezi kujifungua kwenye level ya zahanati watakwenda kwenye kituo cha afya ambacho kinatoa huduma ya upasuaji” aliongezea Simon Nzilibili.
Aidha, kwa mama mjamzito au ambaye ameshajifungua ndani ya siku 42 akipata dharura yoyote ya kiafya apige namba 115 kwa msaada zaidi.
