DAR ES SALAAM; Msemaji wa zamani wa Yanga, Haji Manara, amesema muda sahihi utaongea wenyewe kuhusu kinachoendelea kwenye ndoa yake na Zaiylisa, hivyo wana habari hawana sababu ya kumtafuta kwa sasa.
Manara ameandika kwenye ukurasa wake wa instagramu asubuhi hii:”Waandishi wa habari msihangaike kunitafuta na kunipigia, Jibu langu kwa hili liliotokea ni lile lile moja 𝗡O COMMENTS kwa sasa !!
–
“Nimeamua kukaa kimya ili muda sahihi uje kuongea wenyewe. Nawapenda sana Wanahabari wenzangu, lakini kwa heshma kubwa nawaomba mnielewe msimamo wangu huu. Content hii ubora wake ni ukimya wangu ,zaidi ya kile nilichoandika juzi!!”
–
Wanandoa hao wamekuwa na wiki ya dhoruba ya penzi lao wakitupiana vijembe mitandaoni kuonesha kuwa penzi lao lililokuwa shatashata na kufuatiwa na ndoa iliyotikisa nchi nzima sasa lipo taabani au tayari imesha zama korongoni.
