Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akisaini kitabu cha maombolezo cha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Rukwa, Irene Ndyamkama leo Aprili 27, 2022 katika viwanja vya Bunge, jijini Dodoma.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akitia saini kitabu cha maombolezo baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Rukwa, Irene Ndyamukama, kwenye viwanja vya Bunge, jijini Dodoma, leo Aprili 27, 2022. Wabunge wakisaini kitabu cha maombolezo cha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum, mkoa wa Rukwa, Irene Ndyamkama leo Aprili 27, 2022 katika viwanja vya Bunge, jijini Dodoma. Waziri mkuu Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Dk. Tulia Acksonwamewaongoza waombolezaji kupokea mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti maalum, mkoa wa Rukwa, Irene Ndwamkama, katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma, leo Aprili 27, 2022. Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa wa Viti Maalum, mkoa wa Rukwa (CCM), Irene Ndiyamkama, ukiwasili bungeni, jijini Dodoma kwa ajili ya kuagwa na Bunge.