
MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
Mtaalam wa virutubisho tiba, Abdallah Mandai, ameitaka jamii kujenga utaratibu wa kula mchicha ili kuondokana na maradhi mbalimbali yakiwamo ya kibofu cha mkojo na upungufu wa damu.
Mandai ametaja faida nyingine ya mchicha kuwa unaondoa tezi la shingo, unasafisha damu, unaondoa maumivu ya mgongo, kuharisha, kuhara damu, unatibu matatizo ya ukikojozi, minyoo, unaondoa maumivu ya mwili na ya mgongo.
Mandai ametaja faida hizo za mchicha leo Jumatano, Machi 15, 2023, jijini Dar es Salaam, wakati akizungumzia faida za kutumia aina mbambali za mboga za majani.
“Mchicha unaoweza kuutumia kwa tiba; chemsha maji lita moja na nusu, tia kilo moja ya mchicha, acha ukae dakika tano kisha kunywa kikombe kimoja, kunywa yote siku moja usiyalaze.
“Pia chuma kiasi kidogo cha mchicha, ponda na funga shingoni eneo lenye tezi kila unapolala, muda wa siku tano ni tiba ya tezi la shingo.

“Ponda kiasi kidogo cha mchicha, pasha moto kisha ufunge mahali panapouma, lala nao, joto lake lenye maji litaondoa maumivu yote, fanya hivyo kila siku jioni muda wa siku tano huku kila siku ukiuandaa mpya,” amesema Mtaalam Mandai.
Aidha, ametoa mwito kwa yeyote anayekabiliwa na tatizo la kiafya, aende katika kituo chake cha kutolea huduma za afya, Ukonga Mongo la Ndege, jijini Dar es Salaam ambapo wanamjali mgonjwa yeyote, wanatumia virutubisho tiba asili kuondoa changamoto mbalimbali za kiafya zinazomsumbua binadamu.
