Mkaratusi ni mti wa kupandwa unapatikana maeneo mengi nchini.
Mti huu mrefu wenye majani membamba, uliletwa nchini kutoka Amerika na Ulaya, karne ya tisa.
Mti huu licha ya kutumika kupasua mbao pia una faida nyingi nyingine ikiwa ni pamoja na ni mmea tiba nzuri kwa maradhi ya njia ya hewa.
~Makaratusi pia unasaidia kutibu matatizo ya kifua, malaria sugu, maradhi ya kinywa, baridi yabisi na vidonda.
~Kwa mwenye tatizo la kifua, malaria na baridi yabisi anatakiwa kuchemsha majani ya mti huu kisha ajifushe akiwa amejifunika nguo nzito kama blanket ili mvuke umpate vema mwilini.
~Kwa tatizo la kidonda kausha kivulini majani ya mti huu kisha saga unga wake jipake kwenye jeraha utapata nafuu haraka.
Tiba Nyingine
Katika kurasa nyingine tumejadili magonjwa mbalimbali ikiwemo Kwikwi, pumu, vidonda vya tumbo, tatizo la nyonga na tatizo la Koo na mengineyo mengi.
Ndugu msomaji, uwe huru kuuliza maswali au kutoa maoni yako kuhusu makala hii. Na ikiwa una changamoto yoyote mpigie Mtaalam Abdallah Mandai kwa namba 0745 900600 na hakika utajibiwa kwa wakati muafaka.
