Kisamvu ni miongoni mwa mboga za majani,ambazo inasemekana kuwa ni moja Kati ya mboga zinazopendwa na watu wachache. Licha ya mboga hii kuwa ni miongoni mwa zisizopendwa, inasaidia mambo mengi katika mwili wa binadamu.
Zipo faida nyingi za kula kisamvu na moja ya faida hizo ni,
~Kisamvu kinaongeza damu kwa haraka pengine kuliko aina nyingine ya mboga za majani.
~Mboga hii ina protini nyingi na kiwango kikubwa cha nyuzinyuzi (fibre), inasaidia wanawake wanaosumbuliwa na maumivu ya tumbo wakati wa hedhi.
~Hata hivyo, kwa mjamzito asitumie juisi ya mboga hii isipokua kwa maelekezo kutoka kwa mtaalamu, hii ni kwa sababu ina kiwango kikubwa cha kemikali inayoweza kusababisha mimba kutoka.
~Kwa anayesumbuliwa na tatizo la maumivu ya tumbo wakati wa hedhi aponde mboga hii kisha aanike baada ya kukauka asage unga wake autumie katika maji moto au uji usio mzito.
~Pia juisi ya kisamvu inasaidia kwa wale wenye makohozi yanayoonesha kukaa katika koo muda wote.
Chukua kisamvu kiponde kisha kamua maji yake changanya na asali kunywa inaondoa tatizo hilo.
~Pia mbegu za muhogo ambazo ndizo chanzo cha kisamvu, zikisagwa unga wake utumiwe katika uji usio mzito au maji moto unasaidia kuzibua mirija ya uzazi na kupevusha mayai kwa kinamama wenye tatizo hilo.
~Kwa mwenye maradhi ya kisukari atumie pia katika uji itasaidia kukiweka katika hali ya kawaida.
Ikiwa una tatizo lolote la kiafya karibu katika kituo chetu cha kutolea huduma Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam.
Tunamjali kila mgonjwa na kumpa huduma stahiki. Katika kuhudumia wenye matatizo ya kiafya tunatumia tiba lishe na virutubisho asilia.
Ikiwa unahitaji ufafanuzi wa jambo lolote unaweza kuwasiliana na mtaalam Abdallah MANDAI kwa namba 0745900600 au tembelea tovuti yetu kwa anwani ya www.dkmandai.com
