
Shule ya msingi Lorbene, iliyoko wilayani Simanjiro, mkoa wa Manyara, imeshika nafasi ya mwisho katika matokeo ya mtihani wa darasa la Saba mwaka huu.
Shule hiyo ipo katika kijiji cha Lorbene alichozaliwa mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka.
Kiwilaya imeshika nafasi ya 41 kati ya shule 41, kimkoa ya 215 kati ya shule 216 ambapo wanafunzi 10 walifanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba mwaka huu.
Hata hivyo baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamemtupia lawama mbunge Ole Sendeka kuwa ameaiacha shule hilo bila kuipa msukumu ambapo ingeweza kufanya vizuri.
Saitoti Kimeso amesema mbunge huyo alipaswa kuipa kipaumbele shule hiyo ili ifanye viziri kwenye taaluma na siyo kushika nafasi ya mwisho.
Mkazi mwingine John Mollel amesema mbunge huyo anapaswa kuiga nyayo za mchimbaji maarufu wa madini ya Tanzanite Bilionea Saniniu Laizer ambaye amejenga shule ya mtaala wa kiingereza kijiji kwao.
Hata hivyo, mbunge huyo amesema shule zote za wilaya ya Simanjiro ni zake hivyo hakuna shida shule ya Lorbene kuwa ya mwisho.
