Watu watatu nchini Misri watakamatwa baada ya maelfu ya dozi za chanjo ya corona kutupwa katika mji wa Minya, ulioko kilomita 200 kutoka Kusini mwa mji wa Cairo.
Waendesha mashtaka nchini humo wametoa amri hiyo baada ya picha zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii wiki iliyopita, kuonesha masanduku ya chanjo ambayo hayajafunguliwa yakiwa yametapakaa katika ukingo wa maji.
Mamlaka imesema ni karibu dozi 20,000 za chanjo ya Sinopharm kutoka China yenye thamani ya zaidi ya $300,000 (£220,000), zimepotea baada ya kutunzwa katika kiwango cha joto kisicho sahihi.
Ni asilimia 11 ya idadi ya watu wa Misri ndio wamepata chanjo ya uviko 19 huku nyingine sita ndio wamepata dozi kamili.
