Stelingi wa tamthiria hiyo ya jarida la mapicha alikuwa Lance Spearman, aka Spear, nafasi iliyochezwa na jamaa mwigizaji Joe Mkwanazi, nyota aliyegunduliwa na Stanley N. Bunn, mpiga picha mzungu, wakati Mkwanazi alipokuwa akifanya kazi kama mpiga kinanda katika klabu usiku na mchana akiwa houseboy huko Afrika ya Kusini.
Spear alitamba mno miaka ya 1960 na 1970, katika African Film Magazine lililokuwa jarida maarufu kwa vijana Afrika nzima. Kila toleo lilileta simulizi mpya za Spearman akiwakabili wahalifu, akitatua uhalifu, na kuonyesha ushupavu wa hali ya juu.
Kwa kuwa Jarida hili liliibuka wakati wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, African Film Magazine ilibidi kuepuka kujihusisha moja kwa moja na Afrika Kusini, ambako jarida hilo lilichapishwa awali. Badala yake, ikatumika anuani ya Lagos, Nigeria, ili kuficha asili yake.
Picha zikawa zinapigwa maeneo kama Swaziland, kisha kutumwa London kwa ajili ya uhariri na uchapoishaji, kabla ya kusambazwa kote barani Afrika. Utaratibu huu wa uzalishaji wa kimataifa ulilipa jarida la African Film mvuto wa hali ya juu wa kisinema, huku wasomaji wa Kiafrika wakifurahia hadithi zenye ubora wa hali ya juu
Lance Spearman, maarufu kama “The Spear,” alikuwa zaidi ya mhusika mkuu. Kupitia jarida la African Film Magazine, Spearman alileta hadithi zilizojaa vituko vya kusisimua, mbwembwe za kisasa, na ushupavu ulioweka heshima ya Kiafrika mbele ya ulimwengu.
Spear alikuwa na washirika wa karibu kina Kapteni Victor, rafiki yake mwaminifu wa polisi, na Sonia, mwanamke huru wa kisasa, na mvulana mtukutu Lemmy, wakipambana na wahalifu katili; Rabon Zollo mwenye kiraka jichoni, The Hook-Hand Killer na Dr. Devil
Lakini mwaka 1972
