
Mtaalamu wa Virutubisho Tiba, Abdallah Mandai, amefichua siri ya namna kinamama na dada wanaweza kudumu na ngozi inayovutia wakati wote.
Mandai amesema mara nyingi amekuwa akizungumzia namna ya kutibu maradhi mbalimbali kwa njia asili, leo Novemba 5, 2021, wakati tunaianza wikiendi, ameona azungumzie namna ya kuifanya ngozi ya kinamama kuwa nyororo na ya mvuto kwa njia asili.
“Tumia utomvu wa papai mbichi kuifanya ngozi yako kuwa na mwonekano mzuri na wa kumvutia kila mmoja. Paka utomvu mweupe wa papai bichi mwili mzima.
“Baada ya saa moja oga kisha paka maziwa mtindi mwili mzima ikiwa lengo lako ni kuufanya mwili wako kwa ujumla kuwa na mwonekano mzuri.
“Ni vema fanya hivyo majira ya saa za usiku. Baada ya kutumia njia hii utashangaa kila atakayekuona atavutiwa nawe.
“Au paka parachichi mwili mzima saa za kwenda kulala. Asubuhi oga mwili mzima. Ngozi yako itakuwa na mvuto kwa kila atayekutazama,” amesema mtaalam huyo.
