In this image from video provided by the Ukrainian Presidential Press Office and posted on Facebook early Saturday, March 12, 2022, Ukrainian President Volodymyr Zelenskyy speaks in Kyiv, Ukraine. (Ukrainian Presidential Press Office via AP)

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, amesema mapigano katika jimbo la Lugansk nchini humo kwa sasa ni mazito.
“Hali katika eneo la mapigano haijabadilika. Kwa usaidizi wa vikosi vya kimkakati, jeshi la Ukraine linaimarisha ulinzi katika jimbo laLuhansk – hali kusema ukweli ni ngumu kwa sasa.
“Wavamizi wanaweka shinikizo kubwa kuelekea Donetsk n,” amesema Zelensky kupitia ujumbe wa video.
Kulingana na kiongozi huyo wa Ukraine, katika jimbo la Kharkiv, vikosi vya Warusi vinafyatua makombora mengi.
“Wamejitahidi kwa kila njia kuwazuia wavamizi, lakini jeshi la Urusi halielewi chochote. Linafanya uharibifu tu – kwa njia hii inaonesha makamanda wake hawana msimamo,” amesema Zelensky.
