Na Mtaalam Mandai – 0745900 600
Upungufu wa nguvu za kiume ni hali ambapo mwanaume anashindwa kusimamisha au kudumisha uume katika hali ya ugumu unaotosheleza kufanya tendo la ndoa kikamilifu. Hali hii inaweza kuwa ya muda mfupi au ya kudumu kulingana na chanzo chake.
Wewe ni mtu makini unakumbuka kwamba unahitaji damu ili uume usimame. Unakumbuka pia ili uume usimame, kuna vitu muhimu vinatakiwa viwe sawa ili damu iingie kwa kiwango kinachotakiwa kwenye uume.
Ukweli wa Kusisimua: Usiku Uliotakiwa Kuwa wa Kipekee Uliofanya Nianze Kuandika
Hali hii haimchagui mtu, hata daktari huweza kukutana nayo. Usiku mmoja uliopangwa kuwa maalum sana ukiwa na mke wangu—taa zikiwa za mpororo na kila kitu kikiwa sawa—ghafla wakati wa tukio lenyewe, jogoo alilala fofofo!
Aibu na hofu zilinivamia papo hapo. Moyo ulipiga kwa kasi ya ajabu. Lakini kama daktari, badala ya kupaniki na kukimbilia dawa za mtaani za kutilia shaka, akili yangu ya kitatibu ikashtuka.
Nilifanya uchunguzi wa haraka wa kisaikolojia na kugundua ni athari ya muda mfupi ya dawa fulani niliyomeza mchana kwa ajili ya maumivu madogo.
Baada ya masaa kadhaa kuisha, kila kitu kilirudi sawa kabisa! Hii inakuonyesha kuwa sio kila changamoto inahitaji kumeza vidonge.
Upungufu wa Nguvu za Kiume Unasabishwa na nini? – Sababu Kuu
Vyanzo vya tatizo hili vimegawanyika katika sehemu kuu mbili:
- Sababu za Kimwili: Magonjwa sugu kama kisukari na shinikizo la juu la damu, magonjwa ya moyo na kuziba kwa mishipa ya damu (Atherosclerosis), kupungua kwa homoni ya Testosterone, pamoja na uzito uliopitiliza na ukosefu wa mazoezi.
- Sababu za Kihisia (kisaikolojia):
- Msongo wa mawazo (stress) wa kazini au nyumbani,
- wasiwasi wa kushindwa tendo (Performance Anxiety),
- na sonona au uchovu uliopitiliza wa akili.
3. Dalili za Kukosa Nguvu za Kiume na Dalili za Mwanaume Asiye na Nguvu za Kiume
Ni muhimu kutambua ishara hizi mapema ili kuzuia madhara makubwa zaidi na kuchukua hatua sahihi:
- Ugumu wa kusimamisha uume: Kuchukua muda mrefu sana au kushindwa kabisa kusimamisha wakati wa maandalizi.
- Kushindwa kudumu katika tendo: Uume kulegea haraka mara tu baada ya kuanza tendo au wakati wa kupenya (Penetration).
- Kupungua kwa hamu ya tendo: Kutohisi kabisa hitaji au msisimko wa kushiriki tendo la ndoa kwa muda mrefu.
- Uume kutosimama imara: Kusimama ukiwa “legelege” na kushindwa kuhimili ubora wa tendo lenyewe.
Jinsi ya Kupima Nguvu za Kiume Nyumbani
Kabla ya kukimbilia kutafuta dawa yoyote, unapaswa kujua kiwango chako cha tatizo. Wataalamu hutumia vipimo vinavyoangalia maeneo haya:
- Confidence: Kiwango chako cha kujiamini wakati wa kusimamisha.
- Erection Firmness: Ugumu wa uume wako unapoingia.
- Maintenance: Uwezo wa kuendelea na tendo bila kulegea katikati.
- Satisfaction: Kiwango cha kuridhika kwako na mwenza wako baada ya tendo.
Nguvu za Kiume ni Nini?
Nguvu za kiume ni hali ambapo mwanaume anaweza kusimamisha au kudumisha uume katika hali ya ugumu unaotosheleza kuingia kwenye uke na kufanya tendo la ndoa kikamilifu hadi mwisho.
Nguvu za kiume ni heshima ya mwanaume. Nguvu za kiume humpa mwanaume, hali ya kujiamini, amani katika mahusiano, na kiashiria kikubwa cha afya ya mwanaume.
Nini hutokea mpaka uume ukasimama?
Inabidi ufahamu yanayotokea mpaka uume unasimama na kuwa mgumu kuweza kuingia uke na kufanya tendo la ndoa.
Kinachosababisha uume kusimama na kuwa mgumu ni damu. Windi wa damu kwenye uume → uume mkakamavu.
Damu kidogo kwenye uume → uume legevu. Sasa nini kinasababisha damu kuingia kwenye uume?
Unapopata hamu ya kujamiiana / kupata mhemko, damu huingia kwenye mishipa ya uume kwa kiasi kinachotakiwa.
Mishipa ya fahamu huifungua mishipa hii na kuipanya itanuke. Damu ikiingia hupenya kwenye misuli kiasi cha kuwa mgumu.
Kisha uume hujifunga kutokuruhusu damu kurudi kwenye mzunguko wa mwili. Maana yake ni kwamba kama kuweka maji kwenye pakti ya plastiki na kuifunga.
Itatanuka na kuwa ngumu (kusimama). Ukifungua fundo → maji yatatoka → ile pakti itajifinya kulegea na kuwa ndogo (uume kulala).
Maana yake, unahitaji yafuatayo ili uume usimame:
- ubongo wako kuwa sawa, kupata ashki / kutamani. Yani umtamani mwenza wako. Uume wako uweze kutambua huyu ni wa kumtamani. Usitamani kila mtu (au wewe uume wako unasimama kila unapomuona mwanamke yeyote?) Hapana una mipaka. Yani unatakiwa pia usimame kwa mpenzi wako.
- Mishipa ya fahamu iwe sawa ili iruhusu mishipa na misuli kutanuka – bila hivi damu haiwezi kuingia na kushikiliwa kwenye uume. Uume utakuwa umelala.
- Mishipa ya damu iwe sawa ili iruhusu damu kuingia na kushikiliwa kwenye uume. Ndiyo maana vyakula vinavyotanua mishipa ya damu kama vile tangawizi, asali, vitunguu saumu na maharagwe huongeza nguvu za kiume. Umeona sasa? Unaanza kuelewa hii sayansi. WASILIANA NAMI NIKUELEZE UFUMBUZI AU TIBA YA TATIZO HILIKWA SIMU HIYO JUU>
