
Watu wanaohaingaika kutafuta tiba ya maradhi ya baridi yabisi wametakiwa kutumia ufuta wenye rangi nyeusi kukabiliana na tatizo hilo.
Mtaalam wa Virutubisho Tiba, Abdallah Mandai, ameyasema hayo leo Novemba 11, 2021, jijini Dar es Salaam, wakati akizungumzia namna vyakula vinavyopatikana katika jamii vilivyomsada katika kutibu magonjwa mbalimbali.
“Loweke kijiko kimoja cha ufuta mweusi ndani ya glasi ya maji saa za jioni ulaze hadi asubuhi. Baada ya kumka kabla hujala chochote kunywa maji yote uliyolowekea ufuta huo na malizie kwa kuula wenyewe wote.
“Endelea kufanya hivyo kila siku katika kipindi cha miezi mitatu mfululizo, utaondokana kabisa na tatizo hilo,” amesema Mtaalam Mandai.
Ametanabahisha kuwa mgonjwa wa baridi yabisi hushikwa na maumivu makali kwenye misuli au viungo mbalimbali vya mwili.
Mara nyingi inakuwa vigumu kwa asiye mtaalamu kutofautisha maradhi ya baridi yabisi na jongo (gout).
Aidha, maradhi ya baridi yabisi yasipotibiwa mapema yanaweza kumlemaza mgonjwa.
Wataalamu wanasema baridi yabisi inaweza kutokea baada ya utumbo mkubwa kushindwa kunyonya chumvi muhimu kutoka kwenye mzunguko wa damu au upungufu wa chumvi iitwayo soda fosfeti kwenye chembechembe za mwili.
Ufuta umesheheni madini, protini, carbohydrate, vitamini A, vitamini E, lecithin, kalsiamu, chuma na chromium.
