
Mtaalam wa Virutubisho Tiba, Abdallah Mandai, amesema wakati umefika kwa wanaosumbuka na maradhi ya pumu (athma), kuondokana na mateso.
Akizungumza leo Oktoba Nne, 2021, jijini Dar es Salaam, Mandai amesema mlazalaza mmea asili, umeonesha maajabu makubwa ya kitiba dhidi ya magonjwa mengi ikiwamo pumu.
“Majani ya mlazalaza yenye ladha ya sukari, ndiyo hasa ni tiba ya pumu.
“Chuma majani mabichi ya mmea huu yenye uzito wa nusu kilo, yatwange kisha tengeneza juisi, changanya na mayai matatu ya kuku wa asili, vijiko vikubwa vitano vya asali na ndimu au limau mbili, changanya vizuri mchanganyiko huo.
“Kunywa nusu glasi ya mchanyiko huo kutwa mara mbili, asubuhi na jioni muda wa siku saba. Tiba hii pia inaweza kuondoa sumu mwilini na tatizo la makohozi.
Ikiwa umetumia tiba hiyo na hupati nafuu, karibu kwenye kituo chetu cha kutolea huduma za afya, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam, utapata huduma nzuri dhidi ya matatizo ya kiafya yanayokusumbua.
Kwa asiyefahamu, Pumu ni ugonjwa unaosababishwa na hitilafu kwenye mfumo wa upumuaji. Umekuwa ukiwapata watu wa rika na jinsia zote kwenye maeneo mbalimbali nchini na kwingineko duniani.
