
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru), mkoa wa Njombe imetathmini namna rushwa ya ngono inavyotumika katika sekta ya elimu kwenye halmashauri ya wilaya ya Ludewa na kubaini kutumika hasa katika upangaji wa vituo vya kazi.
Mkuu wa Takukuru Mkoa huo, Kassim Ephrem amesema katika kipindi cha mwezi Aprili hadi Juni Mwaka huu, taasisi hiyo imefanya uchambuzi wa mifumo minne, ambapo halmashauri ya wilaya ya Ludewa rushwa ya ngono imekita mizizi katika idara ya elimu.
Amesema miongoni mwa hatua zilizochukuliwa na taasisi hiyo ni pamoja na kutoa maelekezo kwa viongozi wa sekta ya elimu kufanya ufuatiliaji kwa walimu na upandishaji wa madaraja.
“Tumekaa na viongozi na kuwaomba wazingatie taratibu ya mifumo yao na kuhakikisha haitoi mianya ya vitendo vya rushwa kwa kile wanachokifanya na tutaendelea kufuatilia kwa ukaribu,” amesema Ephrem.
