Klabu ya Simba imeweka rekodi ya kumaliza tiketi zote za sikukuu ya Simba Day siku tatu kabla ya sherehe ya itakayofanyika jumamosi ya terehe 3/8/2024 katika Uwanja wa Benjamini William Mkapa.
Simba wameweka rekodi hii akiivunja rekodi aliyokuwa ameiweka msimu uliopita ya kujaza uwanja huo unaoingiza mashabiki elfu 60 siku mbili kabla ya Simba Day.
Akizungumzia kufikia tamati kwa uuzaji wa tiketi Afisa Mtendaji Mkuu, Imani Kajula amesema, ” Simba tumeonyesha ukubwa wetu na tumeweza kuvunja rekodi yetu ya mwaka jana ambapo tuliuza tiketi zote siku mbili kabla ya Simba Day, mwaka huu tumeuza tiketi zote – SOLD OUT siku tatu kabla ya Simba Day.”
“Hongereni sana mashabiki wetu na tukutane uwanja wa mkapa kwenye Simba Day ya Ubaya Ubwela. Timu yeyote kubwa inapimwa na ukubwa wa sapoti ya mashabiki wake, na hii inadhihirisha kwanini mashabiki wa Simba mlichaguliwa kuwa mashabiki bora barani Afrika.”
Hata hivyo, Mhamasishaji wa Yanga, Haji Manara ameponda na kusema tiketi nyingi wamepewa walanguzi: ” Mgpjeni siku hiyo mtashuhudia watu wakilanguliwa na mtaona mapengo jukwaani,” amesema Manara leo akiwa klabu ya Yanga akiwatambulisha wasanii wa Yanga wakiongozwa na Harmonizer watakaotumbuiza Siku ya Mwananchi Jumapiliijayo.u yao.
