Klabu ya Simba kupitia Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally hiyo imetangaza rasmi kuwa Tamasha la Simba Day litafanyika Agosti 3, 2024 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Kwa kawaida Simba Day hufanyika Agosti 8 ya kila mwaka lakini kutokana na kuwepo kwa michuano ya Ngao ya Jamii siku hiyo wameamua kuirudisha siku nyuma.
