Salim Mwalimu, Devotha Minja Kigaila rasmi wapewa vyeo Chaumma
Waliokua wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) na kundi la G55 ambao walijiengua kutoka Chadema hivi karibuni, leo wamejiunga na chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) na kukabidhiwa kadi zao za chama nav yeo vya juu katika chama.
Aidha kikao kikuu cha Chaumma kinaendelea kuwapokea wanachama wapya na wajumbe wa kikao hicho wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Hashim Rungwe wamejaza nafasi za uongozi zilizokua wazi ikiwemo ya Makamu mwenyekiti na Katibu Mkuu.
Taarifa ndani ya kikao kinachoendelea kinasema katika nafasi hizo zilizokuwa wazi Salum Mwalimu sasa amekua Katibu Mkuu Taifa, Devotha Minja amekaimu nafasi ya Makamu mwenyekiti Bara na Benson Kigaila amekaimu nafasi ya Naibu katibu Mkuu bara. Haijaelezwe kwa nini hao wawili wamekaimishwa nafasi zao.
Wakati sisi tunatoa taarifa hizo Kikao hicho kinaendelea, endelea kufuatilia mtandao huu ili upate Habari zaidi kuhusu Chaumma.
Na Elvan Stambuli GPL.
