
Watuhumiwa wanne Sylivester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Asey katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Lengai Ole Sabaya wameachiwa huru baada ya kuandika barua ofisi ya DPP ya kuomba wakae meza ya makubaliano ili walipe faini na fidia.
Katika kesi namba mbili ya mwaka 2022 ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekua Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, wameachiliwa huru, huku Sabaya akibaki magereza kuendelea na shauri hilo.
Mkurugenzi Msaidizi wa kutenganisha upelelezi na mashtaka Marternus Marandu, amesema Agosti 3, 2022, washtakiwa hao wanne waliandika barua katika ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa serikali kuomba kukaaa meza ya makubaliano ili kuweza kulipa faini na fidia.
