Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amezitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, kutokubaliana na nchi zinazokiuka sheria za kimataifa katika kulinda amani ya dunia, huku akiirejelea Israel kwa kusema inaendeleza mauaji ya kimbari katika ukanda wa Gaza.
Rais Ramaphosa akitoa hotuba yake wiki hii mbele ya viongozi wa Mataifa mbalimbali katika mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) unaoendelea New York, Marekani, Ramaphosa pia amesema hatua zinapaswa kuchukuliwa kama jinsi taifa lake lilivyochukua kwa kuipeleka Israel mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
”Wakati Wapalestina wakiendelea kukabiliwa na mauaji na njaa, tuna jukumu la kufanya, Afrika Kusini imefanya ili kuokoa maisha kwa kusisitiza kwamba mahakama ya haki ya kimataifa lazima ifanye uamuzi ambao utamaliza mauaji yanayotekelezwa Gaza na kwamba ni lazima iishe, na tupo hapa kusema lazima vita visimamishwe” amesema Rais Ramaphosa.
Amesema wanakaribisha na kukubaliana na uamuzi wa mataifa 142 na mengine zaidi duniani kote, yaliyotangaza kuitambua Palestina kama Taifa huru kupitia umoja huo, na kwamba Israel inapaswa kusikia sauti ya mataifa hayo na kufikia suluhu ya kimgogoro kwa Israel na Palestina.
Lakini pia Kiongozi huyo, amezitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kutambua haki ya kujitambua kwa jamii ya Magharibi mwa Jangwa la Sahara pia akisisitiza upatikanaji wa amani katika baadhi ya mataifa ya Afrika kama DRC, Sudan Kusini.
Ramaphosa amebainisha kwamba, azimio la kwanza kabisa la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo Januari 1946, lilitoa wito wa kuondolewa kwa silaha za nyuklia, na ilikuwa ni baada ya mabomu hayo kutumika Hiroshima na Nagasaki nchini Japan na kusababisha athari mbaya kwa binadamu hasa vifo.
Amesema katika miaka ya hivi karibuni hayajafanyiwa makubaliano ya kidunia kufikia udhibiti wa silaha hizo za nyuklia ingawa Afrika Kusini kwa mwaka ujao wa 2026, itakuwa inafanya mapitio ya mwisho ya mkataba unaozuia matumizi ya silaha za nyuklia.
”Huu mkataba unathibitisha kwamba hizi silaha za nyuklia hazina namna nyingine ya kuzidhibiti badala ya kuzizuia kabisa. Nimeshuhudia baadhi ya viongozi wanasimama hapa na kukemea silaha za nyuklia43m
