Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko ya muundo wa Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji na Wizara ya Nishati kwa Wizara hizo kuwa na Makatibu Wakuu wawili kwa kila Wizara, kuteua na kufanya uhamisho wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa ni
i) Kanali Yahya Ramadhani Kido ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera akichukua nafasi ya Bi. Fatma Mwassa; na
(ii) Kanali Donald William Msengi ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara. Kanali Msengi anachukua nafasi ya Kanali Patrick Kenan Sawala ambaye atapangiwa majukumu mengine.
(i) Dkt. Tausi Mbaga Kida ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango;
(ii) Dkt. Fred Matola Msemwa ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Uwekezaji
(iii) Balozi Waziri Rajab Salum ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara. Balozi Salum anachukua nafasi ya Dkt. Hashil Twaib Abdallah ambaye atapangiwa majukumu mengine;
Na Dkt James Mataragio ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wizara ya Nishati anayeshughulikia masuala ya mafuta na gesi asilia huku Mhandisi Felechesmi Jossen Mramba ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wizara ya Nishati anayeshughulikia masuala ya umeme na nishati jadidifu. # Mandai tv
