
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, amemfukuza kazi bosi wa kampuni ya mafuta Bol Ring Mourwel.
Hakuna taarifa iliyotangazwa kueleza sababu ya kufukuzwa kwake na rais, televisheni ya nchi ilisema jana Alhamisi usiku.
Bosi mpya wa Nile Petroleum Corporation (Nilepet) bado hajachaguliwa.
Aidha, bado haijawekwa wazi kama kufukuzwa kwake kuna uhusiano na madai kuhusu kuhamisha fedha za kiasi cha $250m (£182m) katika benki yake binafsi iliyoko Dubai na Khartoum.
Ingawa alikanusha madai hayo, Bol alichaguliwa mwaka jana na kuchukua nafasi ya Chol Deng Thon.
Alichaguliwa kusimamia Nilepet kukiwa na mipango ya kuendeleza sekta ya mafuta na gesi katika taifa hilo.
