
Jeshi la Polisi nchini limesema litazindua kampeni maalum ya mwezi mmoja itakayojulikana kama msamaha wa Afrika inayolenga usalimishaji silaha haramu kwa hiari.
Msemaji wa Jeshi hilo nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP, David Misime amesema uzinduzi wa kampeni hiyo unafanyika leo Septemba 5 kuanzia saa tatu asubuhi katika Viwanja vya Mashujaa mkoani Dodoma ambapo mgeni rasmi ni Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Yussuf Masauni.
Amesema silaha hizo ni zile zinazomilikiwa na baadhi ya watu kinyume cha sheria, ama kwa kutokujua taratibu za kisheria za umiliki wa silaha.
Aidha Misime amesema “Baada ya uzinduzi huo tushirikiane sote kuelimishana kuwa yeyote atakayesalimisha silaha anayomiliki kinyume cha sheria katika muda utakaotolewa na Mhe.Waziri siku hiyo, hatochukuliwa hatua yeyote ile ya kisheria.
