
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis leo anaanza ziara ya siku tatu nchini Kazakhstan ambako atahudhuria mkutano wa kimataifa wa kidini unaowaleta pamoja viongozi wa dini mbalimbali ulimwenguni.
Atakapowasili kwenye mji mkuu wa Kazakhstan, Nur Sultan, Papa Francis atalakiwa na rais Kassym-Jomart Tokayev na wanadiplomasia wengine.
Hiyo itakuwa ni ziara ya tatu ya Baba Mtakatifunje ya Vatican ndani ya mwaka huu wa 2022.
Papa Francis ambaye kwa muda sasa anasumbuliwa na maumivu ya goti yanayomlazimisha wakati mwingine kutumia kiti cha magurudumu, alikwishazitembelea Malta na Canada mapema mwaka huu.
Mbali ya mkutano wa viongozi wa kidini atakaohuhudhuria, Papa Francis anapanga pia kuongoza misa maalum nchini Kazakhstan.
