Mamlaka nchini Kenya imeweka marufuku ya kutotoka nje kwa siku saba (7) kuanzia jioni hadi alfajiri katika baadhi ya sehemu za kaunti ya Nakuru baada ya kuanza kwa ghasia za kikabila kwenye eneo hilo
Inaelezwa kuwa mtu mmoja (1) ameuawa na wengine wanane (8) kujeruhiwa huku nyumba takribani 12 zikichomwa moto kufuatia mapigano ya kikabila huko Tipis na maeneo ya Mwisho wa Lami
Shirika la Habari la kimataifa la Uingereza (BBC) limechapisha taarifa hiyo leo, Jumatatu Septemba 01.2025 ukibainisha kuwa vurugu hizo ambazo zimeibuka tangu Jumamosi ya juma lililopita katika mpaka wa Nakuru -Narok, zimesababisha familia kadhaa kuhama makazi yao baada ya washambuliaji kuchoma moto nyumba na mali
Kufikia jana Jumapili hali ya wasiwasi bado ilikuwa juu hadi kufikia wakazi wa eneo hilo kufunga sehemu za Barabara ya Nakuru -Narok huko Mwisho Wa Lami, wakipinga mauaji hayo na kuitaka serikali kuchukua hatua za haraka kudhibiti
Kufuatia ghasia hizo, serikali imepeleka maafisa wa usalama eneo hilo ili kurejesha hali ya usalama.
