*Mwenyewe asema anatafuta furaha katika penzi lake la mwisho

Mmiliki bwanyenye wa vyombo vya habari nchini Marekani, Rupert Murdoch (92), Machi 20, 2023 ametangaza kumchumbia ofisa wa zamani wa jeshi la polisi, Anne Leslie Smith mwenye umri wa miaka 66.
Murdoch na Smith walikutana kwa mara ya kwanza katika tukio lililofanyika Septemba mwaka jana katika kasri la Murdoch lililopo California.
“Nilikuwa naogopa kuanza mahaba,” Murdoch alisema katika mahojiano na gazeti la New York Post, ambalo ni mojawapo ya magazeti yake.
“Lakini nilifahamu kwamba hilo lilikuwa ni penzi langu la mwisho “Lazima liwe” , “nina furaha”. Murdoch alitalikiana na na mke wake wa nne, Jerry Hall, mwaka jana.
Murdoch alisema alikuwa ” kwa kiwango cha theluthi moja alikuwa na asili ya Ireland” na akamuomba uchumba Smith katika Siku ya Mtakatifu Patrick na anadai alikuwa “mwenye aibu sana”.
Mume wa mchumba wake Smith aliitwa Chester Smith, muimbaji wa muziki wa country na mtangazaji wa redio na televisheni aliyefariki kabla ya wawili hao kuoana.
