
Mtaalam wa virutubisho tiba, Abdallah Mandai, amesema mwarobaini unasaidia kuondoa tatizo la uoni hafifu kwa binadamu hususan wakati wa usiku.
Mandai ameyasema hayo leo Ijumaa Desemba 16, 2022, jijini Dar es Salaam.
“Pondaponda majani ya mwarobaini, ongeza maji kidogo, chuja kwa kitambaa safi.
“Weka matone mawili ya juisi ya mwarobaini katika kila jicho na nyingine paka macho yote. Tiba hii ifanye kila siku jioni baada ya giza kuingia hadi utakapopata nafuu au kupona kabisa,” amesema mtaalam Mandai.
Mtaalamu huyo amefafanua kuwa kutoona usiku mara nyingi kunasababishwa na ukosefu wa vitamini A kwenye vyakula anavyokula kila siku mwathiriwa.
Amesema ili kutibu tatizo mwathiriwa ahakikishe anatumia vyakula vyenye wingi wa vitamini hiyo ambavyo ni pamoja na karoti, bitruti na spinachi.
“Kama una tatizo lolote la kiafya, karibu kwenye kituo chetu cha kutolea huduma za afya, Ukonga Mongo la Ndege, jijini Dar es Salaam.
“Tunamjali mgonjwa yeyote, tunatumia tiba lishe na virutubisho tiba asili kuondoa changamoto mbalimbali za kiafya zinazomsumbua binadamu,” amesema Mandai.
