
Mtaalam wa virutubisho tiba, Abdallah Mandai amewataka kinamama wenye tatizo la harufu mbaya ukeni kutumia mjafari na muomboa.
Amesema mimea hiyo ina uwezo mkubwa wa kukabiliana na tatizo hilo na kurudisha furaha ya mwanamke iliyopotea baada ya kukumbwa na tatizo hilo.
Mandai ameyasema hayo leo Aprili 12, 2022, jijini Dar es Salaam, wakati akizungumzia magonjwa ya kinamama na namna ya kukabiliana nayo.
“Chukua majani ya mjafari na muomboa yachemshe kunywa kikombe cha chai asubuhi na jioni muda wa siku 15 hadi mwezi mmoja.
“Pia unaweza kukausha magome ya mimea hii kisha yasage na tumia kijiko kimoja cha chai cha unga wake kwenye maji moto au uji usio mzito.
“Kunywa siku 15 hadi 30. Aidha kama umebaini una tatizo hilo mwone mtaalamu akuelekeze namna bora ya kutumia mimea hii kwa matokeo bora ya afya yako.
Mandai ambaye ni mtaalam wa tiba ya mimea amewataka watu wanaokabiliwa na magonjwa mbalimbali yakiwamo matatizo ya utasa na ugumba kwenda katika kituo chake cha tiba kilichoko Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam.
