
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Igunga, mkoani Tabora, Fatuma Omary, dereva wake na mtu mwingine, wamefariki dunia katika ajali ya gari.
Ajali hiyo ilitokea jana Jumatano mchana Septemba 14, 2022, katika mteremko wa Inyala, mkoani Mbeya, wakati Mkurugenzi huyo akitoka kwenye kikao cha Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), jijini Mbeya.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Juma Homera amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa chanzo ni uzembe wa dereva wa gari la mkurugenzi aliyekaidi amri ya jeshi la polisi kusimama kupisha msafara wa malori.
Magari mengine yaliyohusishwa katika ajali hiyo ni lori la kubebea mafuta, mali ya kampuni ya Lake Oil na lori la mizigo.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Igunga, Lucas Bugota, amesema alikuwa na Mkurugenzi huyo kwenye mkutano huo, lakini wakati wa kuondoka walisafiri kwa magari tofauti.
