Kiongozi wa kikundi cha uhalifu wa ngono katika Telegram ambacho kilisambaza maelfu ya maudhui ya unyanyasaji wa kijinsia amehukumiwa kifungo cha maisha nchini Korea Kusini.
Kim Nok-wan, 33, alikuwa mkuu wa kundi la Vigilantes, ambalo liliwahadaa waathiriwa ambao walituma picha za utupu na kundi hilo kuzituma katika makundi mengine ya mtandaoni.
Kati ya Mei 2020 na Januari 2025, Vigilantes iliwarubuni watu 261 – idadi kubwa zaidi ya waathiriwa wa unyanyasaji wa ngono mtandaoni katika historia ya Korea Kusini.
Chini ya jina la “mchungaji,” Kim alipatikana na hati ya kutekeleza uhalifu huo ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wadogo na usambazaji wa picha za watoto.
Alihukumiwa Jumatatu baada ya kukutwa na hatia kwa kupanga na kuendesha shirika la uhalifu, kuzalisha na kusambaza maudhui ya kingono na yaliyorikodiwa kinyume cha sheria, matumizi ya maudhui yaliyorikodiwa kinyume cha sheria, na ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia.
“[Kim Nok-wan] amesema mahakamani kwamba anajuta.
Alifanya uhalifu huo katika kipindi cha miaka minne hadi mitano iliyopita,” mahakama ilisema.
“Kwa kuzingatia ukatili wa uhalifu ni muhimu kumtenga kabisa na jamii.”
Kim alitumia wanaume na wanawake kupitia mitandao ya kijamii, akiwavuta kupitia Telegram kabla ya kuwahadaa, kulingana na polisi.
Aliwasiliana na wanaume ambao walionyesha nia ya kuunda au kusambaza picha za uongo, na wanawake ambao walionyesha udadisi kuhusu masuala ya ngono, kisha kutishia kufichua habari zao za kibinafsi au kuziripoti kwa serikali.
Baadhi ya waathiriwa hawa baadaye waliwekwa katika kundi lake kama viongozi.
Kama kiongozi, Kim pia aliwabaka wanawake kumi wenye umri mdogo, akawalazimisha wanawake kufanya ngono na wanaume wengine na kujirekodi akifanya vitendo vya kikatili vilivyosababisha majeraha, polisi waliongeza.
Kesi hiyo ni mara ya kwanza Telegram kushirikiana na polisi wa Korea Kusini, kutoa data zinazohusiana na uhalifu ambazo ziliwezesha uchunguzi zaidi na kusababisha kukamatwa kwa Kim.
Shirika la Polisi la Kitaifa la Korea lilianzisha mfumo rasmi wa ushirikiano na Telegram Oktoba 2024, kuwezesha jukwaa hilo kutoa taarifa muhimu kwa mamlaka.
