
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya, imemwachia huru kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mdude Nyangali aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kusafirisha gramu 23.4 za dawa za kulevya aina ya Heroin.
Hukumu hiyo imetolewa leo baada ya kuahirishwa Juni 14, mwaka huu na kwamba Nyangali ameachiwa huru baada ya kutomkuta na hatia.
Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Zawadi Laizer amesema upekuzi uliofanyika nyumbani kwa mshtakiwa huyo ulikuwa ni batili, haukufuata sheria na kanuni za upekuzi.
