
Jamii imeshauriwa kutumia mbegu za kavumbasi kumaliza tatizo la kuandamwa na pepo mbaya iwapo mtu atakuwa na dalili ya tatizo hilo.
Mtaalam wa Virutubisho tiba, Abdallah Mandai, ametaja dalili za mtu mwenye tatizo hilo ni kujihisi baridi hususan saa za jioni.
Mtaalam huyo ametoa kauli hiyo leo Machi 11, 2022, jijini Dar es Salaam, wakati akizungumzia umuhimu wa mimea tiba.
“Kausha mbegu na maua ya kavumbasi, jifushe pepo au jini iwapo anakuandama atatoweka.
“Na kwa yule anayejisikia homa majira ya saa za jioni akate majani ya kavumbasi, apika kisha ajifukize, pepo, majini na nguvu za giza iwapo kama ilikuwa ni sababu ya kuumwa kwake vitatoweka.
“Ukisaga majani ya kavumbasi yaliyokauka na ukaweka katika uji usio mzito au maji moto unamsaidia mwenye tatizo la hedhi kutokuwa na mpangilio kuwa katika mpangilio.
“Pia mjamzito anaweza kujifungua bila kufanyiwa upasuaji iwapo majani yake akayachanganya katika mboga akala au unga wa majani yake akautumia katika uji usio mzito au maji moto,” amesema.
