
Mama mzazi wa marehemu Hamza Mohammed (pichani), aliyeshambulia na kuua askari wanne kwa risasi kabla ya yeye kuuawa eneo la Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam, Sofia Hassan Askari, amefariki dunia.
Taarifa ya familia inasema Sofia amefariki dunia jana Jumapili, Novemba 7, 2021 na anatarajia kuzikwa kesho saa 7 mchana.
Jina la Askari ni la utani ambalo alipewa kutokana na mume wake kuwa askari (miaka ya nyuma) wakati akiishi katika maeneo ya Upanga jijini Dar es Salaam.
