
Malkia Elizabeth II wa Uingereza, aliyehudumu muda mrefu zaidi katika uongozi wa nchi hiyo kwa takribani miaka 70 amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 96.
Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa kasri la Buckingham. Familia yake ilijumuika pamoja katika makazi yake ya kifalme baada ya wasiwasi kuongezeka juu ya afya yake mapema jana Alhamisi.
Malkia alichukua kiti cha ufalme mwaka 1952 na kufuatia kifo chake, mtoto wake mkubwa Charles, Mwanamfalme wa zamani wa Wales, ataongoza nchi katika kipindi cha maombolezo kama Mfalme mpya.
